Amber Lulu- Napiga Picha za Uchi na Kufanya Vituko Kwaajili Ya Pesa Sio Uhuni

Video vixen maarufu kama Lulu Eugene ‘Amber Lulu’ amefunguka na kudai vituko anavyofanya kama kupiga picha za nusu uchi sio kwasababu ya uhuni bali ni katika harakati za kutafuta maisha mazuri.

Amber Lulu aliyegeukia fani ya muziki amekuwa akitawala vichwa vya habari kutokana na vituko vyake kuanzia na uvaaji wake wa nusu uchi na uongeaji wake na hata tabia yake inayojionyesha mbele za watu.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni Amber Lulu amedai kuwa Watanzania wana kasumba ya kuamini kila kitu wanachosoma juu ya mtu au wanachosikia ila saa nyingine watu wanatafuta njia ya kutokea hivyo njia pekee ya kufanikiwa hilo ni kufanya vituko kama hivyo ili kupata umaarufu.

Jamani kwa mfano mimi nikipiga picha nimevaa nguo ya ndani tu utakuta ni kwa ajili ya kutangaza nguo hiyo sio kwamba najinadi au najiuza kwenye mitandao kama watu wanavyochukulia”.

Ni hivi karibuni tu Amber Lulu ametoka kuwaacha watu midomo wazi baada ya kusema yupo tayari kulala na hats kichaa ilimradi tu anampa pesa na anampenda.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.