Amber Lulu Ni Msichana Mzuri Nimeshamtambulisha Kwa Mama- Prezzo

Mwanamuziki kutoka Kenya, Prezzo amekuwa akishika vichwa vya habari nchini Tanzania baada ya tetesi kusambaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na model na video vixen maarufu kama Amber Lulu.

Miezi michache iliyopita Amber Lulu na Prezzo walionekana pamoja kwenye kumbi mbali mbali za starehe pia kuna picha mtandaoni zikiwaonyesha wakiwa na ukaribu sana ingawa wote walikataa kuwa hawana uhusiano wowote zaidi ya urafiki.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni Prezzo alisema kuwa Amber Lulu ni msichana mrembo na ikitokea siku wakawa wapenzi atakuwa na furaha:

Amber Lulu is a very good friend of mine you know ni mtu ambaye nimejuana naye muda mrefu unajua watu huwa wanachanganya mambo wakikuona uko na msichana wanajua ni mna mahusiano au mandate or something lakini Amber ni rafiki yangu watu wengi hawafahamu kuwa ana roho nzuri sana, ana roho ya huruma na ni mtu anayejali watu wengine hivyo kwakweli mimi sio Mungu siwezi kumhukumu mtu mwingine ila nam-judge Amber Lulu kwa uzuri wake ndio maana mimi na yeye ni mabeste”.

Pia Prezzo aliendelea kufunguka kuwa kama siku ikiwezekana anaweza kabisa kutoka na Amber Lulu;

lakini pia inawezekana siku moja nikawa na uhusiano na Amber Lulu ukitegemea Mimi ni mwanaume na yeye ni  mwanamke halafu ana roho nzuri na ni mrembo kwa nje na ndani unajua watu wanaweza kumuona yupo kwa TV akafanya vituko hivi na vile lakini na yeye ni binadamu so kuna wakati akijisahau amefika ukingoni lakini ana roho safi ndio maana nimeshamtambulisha kwa mama angu na ni marafiki wakubwa na pia mama ni shabiki mkubwa wa Amber Lulu”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.