Amber lulu- Nillan ni Mtoto wa Ivan sio Diamond

Msanii wa mziki wa Bongo fleva, Amber lulu amejikuta akivamiwa na kupewa vichambo vya maana na Team Zari baada ya kusema mtoto wa Zari Nillan sio mtoto wa Diamond.

Siku ya jana Hamisa aliweka picha za mtoto wake aliyezaa na Diamond Instagram na moja kwa moja zilizua gumzo huku kila mmoja akiibuka na kusema lake.

download latest music    

Amber lulu ambaye anajulikana wazi kuwa ni rafiki wa Hamisa aliweka picha ya Nillan huku ikisindikizwa na maneno haya:

Toto Dee raha ya mtoto afanane na na Baba yake kwa kweli maana unaambiwa wako hujafanana naye hata kidole nasubiri wa shoga yangu Gigy Money najua Baba Candy sio mtu wa mchezo mchezo ila hongera mzaa chema”.

Lakini baada ya kuweka posti hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram kuna mtu akamuuliza Yule mwingine kafanana akimaanisha Nillan, Amber Lulu alionekana kajibu Kafanana na Baba yake Ivan mi sipo.

 

Kwa muda mrefu watu wamekuwa wakimfananisha na kudai mtoto wa Zari Nillan hafanani na Diamond na kuunganisha picha huku wakidai Nillan ni mtoto wa Marehemu Ivan jambo ambalo Zari amekwisha kataa na kusema sio kweli na hata Diamond alisema ameshakubali yule ni mtoto wake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.