Angalia Diamond Akijiachia Pamoja na Familia Yake

Mwanamuziki anayefanya vizuri kwenye ulimwengu wa Bongo fleva, Diamond Platnumz yupo nchini South Africa kwa ajili ya kuitembelea familia yake.

Diamond na mpenzi wake Zari ambao wamepitia kipindi kigumu kidogo miezi michache iliyopita baada ya Diamond kuzaa na Hamisa na skendo zisizoisha kila siku za yeye kutembea na wanawake wengine kibao.

download latest music    

Lakini Zari hakumuacha Diamond kwa ajili ya mapungufu yake alikubali kumsamehe na hivi sasa wako wote na furaha tele.

Siku ya Jumatano Diamond alisafiri kuelekea nchini South Africa kwa ajili ya kumsalimia Zari na watoto wao Prince Nillan na Princess Latifah, naomba niseme picha walizoweka mtandaoni zilikuwa nzuri na zilionyesha uhusiano mzuri alionao Diamond na watoto wake hasa Tifah. Baadhi ya picha hizo ni hizi;

Diamond na binti yake Tiffah.
Diamond na watoto wake Nillan na Tiffah.
Diamond, Zari na Watoto wao.
Diamond akicheza na watoto wake.

Diamond ameonekana akifurahi kuwa na familia yake lakini watu wengi wanajiuliza mbona hafanyi vitu hivyo na mtoto wake aliyezaa na Hamisa? Ingawa mpaka Leo haijajulikana nini hatma ya ile kesi waliyoipeleka mahakamani.

Tazama video inayowanyesha jinsi Diamond, Zari na watoto wanavyofurahi:

Diamond ameelekea South Africa kuisalimia familia yake lakini pia ameenda kutengeneza video kwani ameambatana na msanii mwenzake kutoka Wasafi, Rayvanny.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.