Aristotee Aweka Wazi Bifu Lake Irene Uwoya

Aristotee amefunguka na kuweka wazi kuwa hana Bifu na staa wa Bongo movie Irene Uwoya pamoja na kwamba wapo wanaodai hivyo.

Tetesi zilisambaa kuwa Aristoste na Uwoya hawana maelewano Baada ya kumrekodi Dogo Janja akiwa na mpenzi Wake Mpya na kushabikia Penzi hilo wakati akijua wazi alikuwa mume wa Uwoya na ni rafiki yake mkubwa na mteja katika saluni yake.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Aristote alisema hana tatizo lolote na Uwoya kwa sababu alichokiongea kwenye video iliyosambaa ni kweli licha ya kwamba tangu iliposambaa msanii huyo hajafika tena kwenye saluni yake wakati ndiye staa aliyekuwa akitoa mkwanja mrefu kwa kujipamba.

Kiukweli sijisikii vizuri kabisa kupewa hayo majina (Yuda na mnafiki) nina watoto wanakua kesho wakisikia baba yenu alikuwa anaitwa Yuda yaani msaliti inakuwa haileti maana nzuri kabisa, lakini tangu hayo maneno yasambae mitandaoni hajawahi kuja hapa ofisini kwangu, zaidi ya kukutana naye tu mara moja.

Pia isitoshe hii hainipunguzii kitu chochote kwa sababu naamini Uwoya siyo mtu wa kukaa na kinyongo muda mrefu, pia tatizo kubwa ni hawa wapambe ndiyo wanaomjaza maneno lakini yeye mwenyewe hana tatizo na mtu, ingawa mchumba wa Dogo Janja akija tena kutengeneza nywele dukani kwangu nitamsifia kama kawaida na Uwoya naye akija nitafanya hivyohivyo”.

Siku chache zilizopita Uwoya aliweka wazi kuwa hana Bifu na Aristotee ingawa ameweka wazi kuwa hajawahi kuongea naye kwa muda mrefu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.