Aslay Adaiwa Kuanguka Stegini Mjini Kisumu -Kenya.
Msanii wa muziki wa bongo fleva Aslay ameanguka jukwaani baada ya stegi ambayo ilijengwa kwa ajili ya perfomance kuporomoka na kushindwa kuhimili mzigo ulokuwa umebeba.
Hata hivyo baadhi ya waandishi wanadai kuwa hii inaweza kuwa ni mipangi kutoka kwa baadhi ya waandaaji au mtu yoyote ambae hakutaka kumuona Aslay akifanya vizuri katka tamasha hilo.
Matukio ya wasanii wa tanzania kuhariwa show wakiwa nchini kenya yameanza kuripoiwa kwa kushamili sana kiais kwamba inawezekana kuwa kuna figisu kubwa zinazoendelea kati ya wasanii wa Tanzania na waandaji au wasanii wa Kenya.
Aslay alionekana kuanguka mzima mzima katika jukwaa hilo huku akiacha mashabiki wake wakianga kilio kwa kile ambacho hawakutegemea kukiona lakii pia baada ya kukatishwa kwa show hiyo.