Aslay Afunguka Kuhusu Kufananishwa na Rayvanny

Mwanamuziki wa Bongo fleva Aslay anayefanya vizuri kwenye stesheni mbali mbali za redio amefunguka kuwa haoni tatizo mashabiki kumfananisha na mwanamuziki kutoka Wasafi classic, Ray Vanny.

Siku za hivi karibuni kutokana na mafanikio yake anayozidi kuyapata watu mbalimbali hasa mashabiki zake wamekuwa wakimfananisha na wasanii wakubwa kama Diamond na Ali Kiba ambao alidai kuwa hawezi kukubali kufananishwa nao kwa sababu wamemtangulia Sana.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Aslay alifunguka kuwa anaamini Rayvanny ni moja kati ya wasanii wazuri hivyo kufananishwa naye inampa chachu;

Mi naamini mashabiki wenyewe wanapoamua kufanya vitu vyao siwezi kuwapinga lakini kwa upande wangu naweza kusema inanipa chachu ya kufanya vitu vizuri zaidi kwa sababu naamini Rayvanny ni msaanii mkubwa sana ukiangalia mi bado msanii mdogo bado kwa Rayvanny kwa sasahivi naweza nikasema kwa sababu amefika hatua fulani ambayo mi sijawahi kufika na ninatamani nifike hizo level, Kwaiyo wakinipambanisha naye kama tunafanana mi ninaona sawa tu kwa sababu siwezi kumpangia mtu afanye mini alafu isitoshe Rayvanny sio msanii wa kwanza kupambanishwa naye wamenipambanisha na wasanii wengine wakubwa sana lakini niliamini mashabiki walifanya hivyo kwa uzuri tu siamini kama kitendo hiko kilikuwa na ubaya wowote ndio maana sikutaka kufuatilia sana nini kiliendelea baadae lakini mimi sina tatizo lolote”.

Rayvanny kama alivyo Aslay ni mmoja kati ya vijana wenye vipaji vya kupindukia hadi mimi banafsi naamini Ray Vanny anaweza kuwa msanii mwenye kipaji WCB nzima hii inatokana na tungo zake na hata sauti yake ambayo ina utofauti fulani na wasanii wengine wengi wa bongo fleva.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.