Aslay Afunguka Kuhusu Tetesi Za Kuiba Daftari la Nyimbo la Yamoto Band

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri sana kwa hivi sasa Aslay Isihaka amefunguka kwa mara ya kwanza na kuongelea tetesi zilizosambaa mtandaoni kuwa aliiba daftari la nyimbo za Yamoto Band.

Habari hizi zilienea mtandaoni mwaka jana baada ya Kundi la vijana la Yamoto Band kuvunjika. Aslay alikuwa mmoja kati ya wasanii waliounda kundi hili ambalo lilivuma kwa miaka mingi.

download latest music    

Ingawa mpaka leo hii haijajulikana nini has a sababu kibwa iliyofanya mpaka kunsi hill kuvunjika lakini kikubwa kinachisemekana ni masuala ya maslahi yaani uongozi wao ulikuwa hauwapi walichokuwa wanastahili na kusababisha kundi hilo kuvunjika.

Lakini mara tu baada ya kundi hilo kuvunjika na kila msanii kuanza kufanya kazi binafsi Aslay alidhihirisha uwezo wake wa kuimba kwani alianza kung’aa mara moja na alianza kuachia nyimbo zake kwa fujo na nyimbo zake zote zilishika namba moja kwenye chati mbali mbali.

Baada ya kuona kuwa katika muda mfupi ambao Aslay amekuwa peke yake amekuwa akitoa nyimbo nyingi kiasi like ndipo tetesi zilanza kusambaa kuwa Aslay aliiba daftari la nyimbo la Yamoto band lililokuwa na by nyimbo zilizo andikwa na wasanii wotenwakundi hilo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5 Aslay amekana tuhuma hizo na kuhakikishia watu kuwa nyimbo zote anazoimba ni zake:

Hizo tetesi za mimi kuondoka na daftari la Ya Moto Band zilikuwa ni tetesi tu unafikiri zilikuwa na ukweli wowote hapana hazina ukweli yalikuwa ni maneno tuu yaliyoanzishwa na mashabiki ili mradi tuu kuchekesha watu na mimi nilivyoona nilicheka tu maana nilijua ulikuwa ni utani kutoka kwa mashabiki”.

Aslay amekiri kuwa tangu ameondoka katika kundi la Yamoto Band ametoa nyimbo kama kumi na sita na sababu kubwa iliyomsukuma kutoa nyimbo nyingi katika kipindi kifupi ni ili akifanya shoo zake asitumie nyimbo za Yamoto.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.