Aslay Atangaza Kubadilisha Staili Ya Kutoa Nyimbo

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amefunguka na kudai kuanzia sasa anataka kuanza kubadilisha staili aliyokuwa anatumia kutoa nyimbo zake.

Tangu Aslay atoke Yamoto Band alikuwa msanii wa kwanza kupata mafanikio makubwa hasa baada ya kuanzisha trend ya kutoa nyimbo kwa mfulululizo ambapo alitoa nyimbo mara kwa mara.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Enews cha East Africa Tv, Aslay amedai hivi sasa ameamua kubadilisha mtindo huo na kuamua kuzipa nyimbo muda anapotoa kwa sababu kuna wasanii wameiga mtindo huo.

Siwezi nikawa nafanya kitu ambacho naona watu wengi wanang’ang’ania kufanya hivyo sahivi kilichobaki nimeamua natoa wimbo halafu nasikilizia mashabiki wameupokeaje”.

Aslay amesema pia sababu nyingine ya kubadilika ni uongozi wake mpya;

Lakini pia nimebadilika kwa sababu nipo Kwenye management mpya kwaiyo nawasikiliza wanasemaje halafu siwezi nikakurupuka kama zamani kwa sababu nataka muziki wangu uende kimataifa zaidi”.

Wasanii kadhaa walionekana kuiga mtindo wa Aslay wa kutoa nyimbo mfulululizo mfulululizo ingawa wasanii hao walikiri kuwa hakufanikiwa mfano ni Msami Baby.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.