Aslay Atoa Siri Yake Ya Kutoa Ngoma Kali Mara Kwa Mara

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amefunguka na kutaja siri ya mafanikio yake inayompelekea kutoa nyimbo kali kila siku.

Aslay alianza kupata umaarufu katika kundi la Yamoto Band miaka ya nyuma kidogo amezidi kung’aa Zaidi baada ya kuondoka katika kundi.

download latest music    

Aslay ameweza kuwa msanii pekee ambaye amekuwa akitoa nyimbo mara kwa mara na zote zimekuwa ni hit baada ya hit kitu ambacho hakiwezi kufanywa na wasanii wengi Bongo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Aslay amefunguka na kudai siri ya kuwa na nyimbo kali ni katika uandishi ambapo anazingatia kuzungumzia maisha halisi ya watu hasa ambao anaishi nao.

Mimi nikiwa naandika sana naangalia maisha ya kweli ambayo yanayotokea kila siku alafu mimi nimetoka uswazi hivyo naangalia vitu vingi vya uswahilini kwaiyo ni vitu ambavyo vinanipa mimi mashairi mazuri.

Lakini pia kuna baadhi ya mambo sio lazima yanitokee mimi yanaweza kuwatokea watu wengine ila cha muhimu viwe ni vitu vya Ukweli”.

Aslay atakuwa mmoja kati wasanii ambao watafanya show katika Tamasha la Sport&Music Festival mkoani Mwanza,

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.