Aslay- Kifo Cha Masogange Kilizima Wimbo Wangu

Mwanamuziki wa Bongo fleva Isihaka Nassoro maarufu kama Aslay amefunguka na kuelezea jinsi Kifo Cha marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’ kilivyozima wimbo wake.

Aslay ameongelea jinsi wimbo wake wa ‘Kwa raha’ ulivyoshindwa kuvuma kutokana na kutoka kipindi kibaya ambacho ilikuwa ni msiba wa marehemu Masogange.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Aslay amesema kuwa ngoma hiyo aliitoa kama zawadi kwa mashabiki wake kwani ngoma yake ya mwisho kutoa rasmi ni Nibebe mara baada ya kubadilisha mfumo wake wa kutoa ngoma.

Kwa Raha nilitoa kama zawadi kwa sababu kuna ngoma inakuja kuitoa tena baadaye ila nasema ni ngoma yangu naipenda na namshukuru Mwenyenzi Mungu imeenda japo kuwa hapa kati imekutana misukosuko, Agness amefariki, kuna vitu kibao vimetokea lakini nashukuru ngoma hivyo hivyo inaenda“.

Aslay ni msanii mwenye mafanikio sana kiasi ya kwamba kila nyimbo anayotoa inafanya vizuri lakini  wimbo huu wa kwa raha haujafikia mafanikio wa nyimbo zake nyingine kutokana na kutoka wakati ambao kila mtu alikuwa na majonzi ya Masogange.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.