Aslay- Muziki Unanifanya Nakuwa Bize

Staa wa muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amefunguka na kusema anajiona kama mtu anayeishi kama roboti kutokana na kufanya kazi mfululizo.

Aslay ambaye amekuwa kwenye chati toka aondoke Kwenye kundi lake la Yamoto Band ameendelea kufanya vizuri na nyimbo zake kama Nibebe, Natamba na nyinginezo.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Aslay amefunguka kuwa anaamini muda wa kupumzika kwa mwanadamu ni pale anapoondoka duniani, kwa hiyo kila siku yupo studio, kama siyo studio yupo lokesheni anafanya video na kama siyo lokesheni basi yupo kwenye shoo majukwaani.

Sina muda wa kupumzika, kwa maana ninaamini mtu kupumzika ni pale anapofariki dunia, nafanya kazi kila siku ili kuhakikisha nasonga mbele kwenye maisha yangu”.

Aslay anategemewa kupanda stejini moja na mkali kutoka NIgeria Davido pale next door Arena siku ya tarehe 16 Kwenye 30 Billion concert.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.