Aslay Ndani Ya Penzi Zito na Mrembo Mwingine

Staa wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Nibebe’ Aslay Isihaka ameweka wazi penzi lake zito na Mrembo ambaye ni Muigizaji wa Bongo movie Diana Kimary.

Wiki chache zilizopita Aslay alithibitisha kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Tessy Chocolate  ambaye pia ni mama wa mtoto wake mmoja wa kike anayeitwa Moza.

download latest music    

Aslay na Tessy hawa kuweka wazi sababu za kuachana lakini kila mmoja alisisitiza wameachana kwa wema na hawana chuki baina yao.

Siku ya jana Aslay amemuanika Rasmi mpenzi wake Mrembo Diana Kimary Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amemposti mara mbili huku akionyesha wazi kuwa wana Mahusiano zaidi ya urafiki.

Kwenye picha hizo Aslay alisindikiza kwa maneno kama “Mashallah” na “Sasa ndio nini Mke wangu”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.