Aslay- Pesa Ninayo Lakini Sina Utajiri wa Kutisha

Staa wa muziki wa Bongo fleva na hitmaker wa Natamba Aslay Isihaka amefunguka na kuweka wazi kuwa pesa anayo kidogo japo sio pesa kubwa kiasi hicho lakini angalau anayo.

Aslay ni moja kati ya msanii  ambaye amekuwa  akifanya  vizuri sana Kwenye ulimwengu huu wa Bongo fleva kwani amekuwa akitoa hiyo kwa kila nyimbo yake anayoweka mezani.

download latest music    

Hivi karibuni Aslay aliwekwa kundi moja na wasanii wakubwa kama Diamond na Ali Kiba na kusemwa na yeye anaingia Kwenye listi ya wasanii walio na mkwanja mrefu Bongo.

Kwenye Interview aliyofanya na Millard Ayo Tv, Aslay alisema kuwa hawezi kujisema ana hela kubwa lakini anayo pesa ya kubadilisha mboga ya kawaida:

Of course hela ya kubadilisha mboga ninayo Alhamdulilah siwezi nikasema sina nitakuwa naongopa hela ninayo lakini sina utajiri wa kutisha”.

Aslay alisemekana ana mkwanja mrefu sana baada ya miezi michache nyuma kununua ndinga la maana lenye viwango vyake aina ya BMW.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.