Aunt Ezekiel aeleza sababu zake za kutotokea kwenye Bongo Movies

Aunt Ezekiel ambaye ni muigizaji wa movie za Bongo hivi karibuni amefunguka kueleza mbona haonekani kwenye movie hizi Kama kitambo.

Mose Iyobo na Aunty Ezekiel

Mrembo huyo ambaye ni mama ya mtoto mmoja na mpenzi wa dancer kutoka Wasafi Records hivi karibuni alifunguka kudai kuwa anapumzika kwa sasa lakini hivi karibuni. Aunt Ezekiel alikiambia kipindi cha Twenzetu cha Times FM.

download latest music    

“Bongo Movie tunaweza kusema ni kama maisha ya binadamu, kuna time analala, anaamka, anapika, so kunakuwa na kazi tofauti tofauti. Naweza kusema kwa sasa hivi Bongo Movie ni muda wetu wa kurelax kwanza kwa hiyo tumepumzika, tumelala tukishaamka nadhani tutakuja na vitu vingi vya tofauti.”

Aliongeza,

“Sio kwamba tukilala ndio hakuna kitu ambacho kitakuja kikubwa zaidi au hakitachukua akili za Watanzania tena, hapana kulala kwa Bongo Movie ni kulala kwa kujipanga ili tunapokuja kurudi tena turudi vizuri, so mimi siamini kama Bongo Movie imekufa, tumerelax tu,”

Hata hivyo aliyekuwa rafiki yake wa karibu Wema Sepetu amekuwa akiachia projects zake mpya pole pole.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua