Aunty Ezekiel Afungukia Mipango Ya Ndoa na Iyobo

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali Aunty Ezekiel amefungukia mipango ya ndoa yake na mpenzi wake na Baba watoto wake Mose Iyobo.

Aunty ameweka wazi kuwa siri kubwa ya Mahusiano Yake na Mose Iyobo kudumu kwa muda mrefu ni kuheshimiana, kusikilizana na kutoleteana ustaa wanapokuwa nyumbani.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni na kituo kimoja cha habari, Aunty amefungukia mipango ya ndoa na Iyobo:

Mamboya ndoa mwanaume ndio anayeamua, Lakini pia kufunga ndoa ni makaratasi tu kikibwa ni jinsi gani unaishi na mpenzi wako na mna maelewano kwa kiasi gani”.

Lakini pia Aunty ameweka wazi kuwa pamoja na kwamba yeye na Iyobo wana uhusiano mzuri lakini wamepitia mambo magumu kwani ameshawahi kumfumania na mwanamke mwingine Lakini pia amekiri ameshawahi kukutwa na meseji za mwanaume mwingine.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.