Aunty Ezekiel Amwaga Mamilioni Kusheherekea Birthday Yake Dubai

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Aunty Ezekiel anadaiwa kumwaga mamilioni ya pesa kwa ajli ya tu ya kuweza kusheherekea birthday yake nchini Dubai.

Global Publishers wanaripoti ya kwamba Aunty hakwenda peke yake Dubai bali aliambatana na mwanaye Cookie pamoja na ndugu zake watatu ambapo wameonekana wakiponda raha katika viwanja mbalimbali nchini humo.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Gazeti la Risasi Mchanganyiko kwa njia ya simu kutoka Dubai, Aunty alianza kwa kusema kuwa, ameamua kufanya sherehe hiyo ya kuzaliwa nje ya nchi ikiwa ni moja ya kufurahia kutimiza miaka 30 akiwa tayari na mtoto wake.

Nilipenda hii iwe ya tofauti kidogo na nilihitaji kufurahi na familia pekee ndiyo maana niliondoka na vijana wangu wawili na mdogo wangu pamoja na mtoto wangu kwa kweli nimeifurahia sana.

Lakini kwa mahesabu ya haraka haraka nauli za watu wanne pamoja na mtoto wangu Cookie inakaribia shilingi milioni tano, gharama za hoteli ni shilingi milioni nne na ushee na kuhusu sherehe hiyo kwa maana ya vyakula na vinywaji  haikuwa kubwa sana ilikuwa  takriban shilingi milioni 2″.

Lakini pia Aunty alizima tetesi za kuwa ameachana na baba watoto wake Mose Iyobo ambaye hakuonekana kabisa kwenye safari hiyo na kupelekea tetesi za kuachana;

Watu wanasema sana kuona nimeenda peke yangu bila Iyobo lakini mbona inawezekana kabisa kitu hicho maana bado kuna vitu vingi tutakuwa pamoja tu”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.