Aunty Ezekiel Awataka Wanawake Waangalie Mapenzi Ya Kweli na Sio Pesa

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Aunty Ezekiel amefunguka na kuwaombea wanawake juu ya tabia ya kupenda kuwa na wanaume wenye pesa bila ya kijamii kipimo cha mapenzi na upendo wao.

Aunty Ezekiel amewashauri wanawake wenzie wenye tabia ya kuangalia kipato cha mwanaume au aina ya kazi kwa mwanaume kabla ya kujiingiza kwenye mahusiano, waache tabia hiyo na badala yake waangalie zaidi mapenzi ya dhati.

download latest music    

Akiongea kwenye usiku wa fainali ya Jibebe Challenge, Aunty amesema kwenye mapenzi hakuna haja ya kuangalia pesa wala kazi na ndio maana hata yeye akaamua kuolewa na Mose Iyobo.

Aunty Ezekiel ameongea hayo kutokana na kupitia mambo hayo kwani miaka ya nyuma alikuwa Kwenye Mahusiano na Jack Pemba ambaye ni mfanyabiashara tajiri sana lakini alishindwa kukaa Kwenye Mahusiano kutokana na kipigo alichokuwa anapata mpaka kupelekea ujauzito kuharibika.

Baada ya kuachana na Jack Pemba ambaye yupo nchini Uganda kwa sasa Aunty amejikuta Kwenye Penzi la Mose zito o ambaye ni dancer wa Diamond Platnumz.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.