Aunty Ezekiel Awatolea Povu Wanawake Wanaojigonga Kwa Iyobo

Mwigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amewatolea povu wanawake wote wanaojigonga kwa mpenzi wake na baba wa mtoto wake Moses Iyobo.

Kupitia ukurasa wake Instagram Aunty amefunguka kuwa kuna wanawake wamekuwa wakimtumia meseji za kimapenzi Iyobo wakati wakijua wazi yupo kwenye uhusiano na ana familia tayari.

download latest music    

Aunty Ezekiel aliandika haya kwenye ukurasa wake wa Instagram;

“Naomba nisema maana nimekaa nalo rohoni naona nashindwa siwezi kuvumilia kidudu mtu kuja kuharibu familia yangu kirahisi kama ulivyodhani mala** wa mji wewe koma uliza kabla hujavamia wanaume wengine hutokaa ujisamehe, kwa uhandsome gani alionao huyu sahivi mkajifanya kutwa kumtongoza kama sio tu ilimradi umeshare na fulani sasa mimi sio mzungu ndugu yangu ntakukanyaga hutaamini kamuulize yule mwanamke wa China akupe habari yangu. Watu gani hamjui kusafisha wako ukatulia mbona hamkumfata alipokuwa mabonde kuinama na tulivyoanza wote mlijifanya kushangaa sahivi kutwa mnapishana inbox kumtongoza”.

Aunty Ezekiel alimuacha mume wake aliyeenda jela na kuzaa na Moses Iyobo ambaye ni mmoja Wa mcheza shoo wa Diamond.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.