Aunty Ezekiel Kuhusu Ugomvi Wake na Iyobo “Hata Vikombe Vinagongana”

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka kuhusu ishu ya ugomvi wake na mpenzi wake pia baba watoto wake mcheza shoo kutoka WCB, Mose Iyobo.

Aunty Ezekiel na Iyobo wamekuwa kwenye mahusiano sasa kwa muda wa miaka minne name kwa pamoja wamezaa mtoto mmoja anayeitwa Cookie, lakini couple hii sio zile za kupenda kiki mitandaoni kwaiyo ilivotokea Aunty kurusha dongo mtandaoni wengi walishtuka.

download latest music    

Wiki iliyopita Aunty Ezekiel alizua gumzo mtandaoni baada ya kuweka posting yenye utata mtandaoni iliyoashiria kuwa yeye na mpenzi wake Mose Iyobo wapo kwenye migogoro fulani hivi.

Baada ya posti hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii tetesi zilisambaa labda huenda Aunty na Iyobo tayari wameachana kutokana na michepuko.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo TV Aunty alifunguka na kudai kuwa kwenye mahusiano kugombana ni kawaida kwa sababu wote ni binadamu:

Unajua waswahili wanasema hata vikombe vinagongana kabatini kwaiyo mimi na Mose pia ni binadamu tuko pamoja kwa miaka minne sasa sidhani kama ni kitu kidogo ambacho kitaweza kupita bila kukwazana kwaiyo ndio kama binadamu ni jambo la kawaida kuna muda ananikwaza lakini na uhakika na mimi pia huwa namkwaza kama binadamu lakini mimi ni mtu ambaye sipendi kuweka mambo yangu mtandaoni lakini hiyo siku nilikuwa nimekwazika sana mpaka nikafika mwisho lakini tulishasemehana na tumeyamaliza”.

Aunty Ezekiel amesisitiza kuwa  hapendelei kuanika mambo yake mtandaoni lakini pia hata kwa marafiki kwani hana kawaida ya kuwaambia hata marafiki zake wa karibu mambo yake binafsi.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.