Aunty Ezekiel na Mose Iyobo Wadaiwa Kutibuana Mtwara

Muigizaji wa Bongo movie na Mjasiriamali Aunty Ezekiel amedaiwa kutibuana na Mpenzi Wake ambaye pia ni baba Watoto Wake dansa kutoka WCB Moses Iyobo.

Sakata kati ya wawili hao lilichukua nafasi mkoani Mtwara ambapo Aunty Ezekiel aliambatana na timu nzima ya WCB kwa ajili ya kufanya tamasha la Wasafi Festival.

download latest music    

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa Aunty Ezekiel na Iyobo walizua sintomfahamu baada ya kudaiwa kufikia hoteli tofauti na kuwa wanapishana bila kusalimiana. Kufuatia hali hiyo mmoja wa watu wa ndani wa Wasafi aliling’ata sikio Ijumaa Wikienda kuwa, wawili hao hawakuwa sawa kwani walikuwa wametibuana.

Hata hivyo, baada ya wawili hao kuwekwa chini na watu wazima waliokuwa kwenda msafara huo, wawili hao hatimaye walionekana pamoja katika mapozi ya kimahaba, hali iliyoonesha mambo kukaa sawa huku wakionekana wakiongea kwa muda mrefu.

Baada ya sakata hilo gazeti hilo lilimsaka Mose Iyobo kwa mahojiano zaidi ambapo alikana tuhuma hizo na kufunguka:

Nani amesema tumetibuana? Siwezi kuongelea hilo tafadhali ni mambo binafsi na yatabaki hivyo,”.

Aunty Ezekiel na Iyobo wamekuwa wakiandamwa na tetesi za kuachana kwa miezi kadhaa sasa juju chanzo kikisemekana kuwa Iyobo na michepuko nyingi.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.