Aunty na Rammy Wajibizana kwa Sababu ya Rambirambi ya Agness

Kumekuwa na figisu figisu nyingi kuhusu rambirambi ya mwanadada agness masogange aliyefariki wiki chache zilizopita huku wakimtuhumu  kiongozi wao  steve nyerere ambae anasemekana kuwa ndie aliyekula  pesa hizo.

Ingawa Steve Nyerere  aliwajibu na kusema kuwa rambi rambi ya marehemu haitakabithiwa kwa ndugu wa marehemu kwa sababu marehemu alikuwa na mtoto aliyekuwa anamtegemea na alimwacha akiwa anasoma hivyo pesa hiyo atakabithiwa mtoto na sio ndugu wa marehemu ikifika 40.

download latest music    

Sasa sakata lingine linakuja baada ya aliyekuwa ex wa Masogange( Rammy Galis)  kuamua kuto ayake ya moyoni kuhusu swala hilo la rambi rambi na kusema kuwa anasikitika sana kuona kuwa michango hiyo haijafikka kwa walengwa na kusema kuwa atajitahidi filamu waliocheza wote inaawanufaisha familia yake.

@rammygallisofficialsintofahamu ya michango ya msiba wako zinanisikitisha sana , namuomba Mungu anisaidie ili niweze kutoa kile  kitaachobarikiwa kwa kazi ya mikono yako na wangu (HUKUMU) , Sania yupo kwa niaba yako.

Baada ya kuandika hivyo Aunty Ezekiel nae alionekana kukwera na maneno hayo na kuamua kumjibu Rammy kwa kusema kuwa aache tabia ya kuwa  na drama na kuwahumiza wafiwa.

Wewe ulitoa shingapi kwenye huo msiba , punguzeni drama basi kwenye mambo ya familia za watu  tena wenye majonzi bado.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.