AY Afunguka Kuhusu Kuhamisha Makazi Marekani

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva Ambwene. Yesaya maarufu kama AY amefunguka na kuweka wazi kuwa amehmisha makazi yake kufika Tanzania kwenda Marekani.

Global Publishers wanaripoti kuwa AY ameweka makazi nchini humo baada ya kununua nyumba ya kifahari nchini humo Miezi michache iliyopita.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers  AY mwenye makazi katika Jiji la Calabasas, California amesema ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu kwamba siku moja awe na makazi kwenye taifa hilo mbali na alipozaliwa Tanzania.

Siri ya kuja kuishi Marekani ni kwamba hii ilikuwa ndoto yangu ya muda mrefu niwe na makazi huku. Kwa hiyo kwa kufanikisha kununua mjengo Marekani kwangu nimetimiza jambo moja muhimu sana maishani mwangu na ninamshukuru Mungu”.

AY na mke wake Remmy walifanikiwa kuzaa mtoto wao wa kwanza siku ya jana ambapo mtoto huyo pia amezaliwa nchini Marekani.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.