Ay Akiri Kuteswa Na Bifu Lilikowepo Kati Ya Fa Na Jay Dee

Msanii mkongwe kutoka nchini Ambwene Yesaya ambae kwa jina la muziki anajulikana kama Ay, amefunguka na kuongelea jinsi ambavyo bifu la wasanii wenzie Mwana Fa na Lady Jay Dee kukaa muda mrefu bila kuelewana wala kufanya kazi pamoja  ilivykuwa ikimpa ugumu wa kushirikiana nao wote wawili ilhali wote walikuwa ni watu wake wa karibu.

Akiongea wikiend hii msanii huyo anasema kuwa pamoja na kwamba kitu hicho kilikuwa kikimsumbua kwa sababu wote walikuwa ni watu wake wa karibu hivyo ilikuwa ikimpa muda mgumu sana lakini alikuwa akiamini kuwa ipo siku watu hao watakuja jupatana ingwa walikuwa hawaongei kabisa.

download latest music    

“Ilikuwani ngumu kwa sabau wote walikuwa hawaongei alafu kwangu wote washikaji kwaiyo ukiongea ukamletea za huyu anakwambia haaaa hayo mambo yaache, lakini ikafika time wakwa wakiuliziana e bhana huyo vipi.. nikasema basi mambo yatakuwa sawa tu”  alifunguka Ay.

Akiongea katika kituo cha East Africa Television, Mwana Fa pia alifunguka na kusema kuwa ” Tupo kwenye ground nzuri,jide ni mshikaji wangu na hata hdugu pia huwa wanakosana , na kila mtu anajua, ila kilichotokea kilishatokea tunaviacha vipite tu, tumefika mahali sasa hivi tunaongea vitu vya kawaida kabisa”

Mwana Fa, Ay na Fid Q wamekuja na project mpya wa kuimba pamoja wimbo wao mpya unaojulikana kama upo hapo, hivyo kwa sasa wasanii hao wanategemea kuwa karibu na kuonekana pamoja katika baadhi ya kazi.Hivyo pia Fid Q alipata nafasi ya kuongelea  mahusiano mapya ya  Mwana Fa na Lady Jay Dee.

‘i tink watu wamezoea kusema keep the good music alive lakini mimi nasema yeye kuwa rafiki na jide tena ni keep tha positive music alive” alisema Fid Q

Mwana Fa na Lady Jay Dee walikuwa katika ugomvi wa muda mrefu na walikuwa hawafanyi kazi tena kama zamani, lakini hivi karibuni wawili hao wameoneana kumaliza tofauti zao na kuona kuna umuhimu wa kufanya kazi pamoja kama zamani, hii ilidhihirika baada ya Mwana Fa aliposapoti wimbo wa mwanadada huyo kwa kuweka katika ukurasa wake wa instagram

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.