B-12 Atabiri Kifo Cha Bongo Fleva Kwa Kiki za Wasanii

Mtangazaji wa kipindi cha XXL cha Clouds Fm Hamisi Mandi maarufu kama B-12 amefunguka na kudai kuwa muziki wa Bongo fleva utakuwa kutokana na kiki za wasanii.

B-12 amedai kuwa kuna dakika mbaya ambazo amekuwa akiziona kama mdau mkubwa wa muziki huo ambapo kiki zimekuwa kubwa na kusababisha muziki kuwa mdogo.

download latest music    

B Dozen amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Bongo 5 ambapo amekiri kuwa muziki wa Bongo fleva kwa sasa unapotezwa na kiki nyingi za wasanii huku akidai wakenya wameanza kuja juu kwa kasi kwenye soko la muziki.

Muziki wetu wa Tanzania umefika sehemu nzuri sana lakini nahisi kama hizi kiki zinazoendelea zitaweza kushusha mziki wetu na hata nilivyoangalia nimegundua kuwa Wakenya sahivi wanarudi kwa kasi sana ambao walikuwa juu sisi tukawaondoa wanaweza wakachukua nafasi kwa sababu ya sisi kuendekeza kiki kwaiyo kwa watu wa media tusapoti mziki mzuri tutafika mbali zaidi”.

Wasanii wengi wamekuwa wakitumia kiki kwa ajili ya kutangaza kazi zao jambo ambalo limekuwa likisemwa kuua mziki wao.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.