Baada ya Akaunti Yake Kuibiwa, Wema Amtuhumu Mange Kimambi.

Siku chache zimepita tangu akaunti ya instagram ya msanii Wema Sepetu kuibiwa na watu wasiojulikana na kuitumia kwa ajili ya mambo mengi ikiwemo biashara, hata hivyo wapo waliokuwa wakionyesha kusikitishwa na kuibiwa kwa akaunti ya mwanadada huyo lakini kitu cha kushangaza ni kwamba Wema Sepetu amemshtumu mtu wa kwanza kufanikisha kuibiwa kwa akaunti hiyo kuwa ni  mwanaharakati anaefanya shughuli zake katika mitandao ya kijamii Mange Kimambi.

Wema na Mange Kimambi wamekuwa marafiki kwa muda mrefu tangu kipindi Wema anataka kushiriki mashindano ya urembo mwaka 2006, na rafiki huo ulidumu kwa muda mrefu mpaka pale wema alipohama chama kwa mara ya pili kutoka chama cha upinzani na kurudi chama tawala, kitu hicho kilimfanya mange amuanike wema kila kitu ingawa hata huku nyuma alikuwa akifanya hivyo.

download latest music    

Wema Sepetu baada ya kuibiwa akaunti hiyo,w=mange kimambi aliweka katikaukurasa wake kuwa anamuomba mtu ali-hack akaunti ya wema aifute tu akaunti hiyo kitu ambacho kimemuumiza sana wema sepetu.

Akilalamika kupitria applictaion yake inayopatikana playstore, wema sepetu amemuomba mange kimambi kumuachia na kumrudishia akaunti hiyo kwa sababu ndio inayompana kumuuzia bidhaa zake na biashara anazofanya.Lakini pia wema amefanya hivyo ili kuonyesha kuwa anamjua mtu anaemchezea na kucheza akaunti yake.

Hata hivyo baada ya kutoa malamiko hayo , mange kimambi alikanusha ku-hack akaunti ya wema sepetu na hata kusema angekuwa anamjua mtu huyo aneweza kumsaidia.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.