Baada ya Davido, Joh Makini Kufanya Kazi na Ice Prince

Mwanamuziki Joh Makini anazidi kupanua wigo wake wa kimuziki kwa kutaka kufanya kazi na ice prince kutoka Nigeria. tetesi za  hapo awali zilikuwa ni Joh Makini kufanya kazi na Davido lakini mambo yanazidi kuwa mazuri kwa kuendelea kufanya vizuri hasa baada ya kutegemea kufanya kolabo nyingine na Ice Prince.

Akiongea na JJ wa Jembe fm , Joh Makini anasema kuwa waliamua kufanya wimbo na Ice Prince pamoja lakini hakutaka kuweka mambo wazi kwa sababu yeye ndie alietafutwa na hii imetokea kama ilivyotokea kwa msanii Davido.

download latest music    

Kuna mtu mmoja tulifanya nae kazi anaitwa eze, tulikutana nae bongo alipokuja kufanya kazi zake ndipo aliniambia kuwa anfanya  kazi na ice prince  na akaniambia kuwa kuna kitu anadhani ni vyema tukafanya nae na mimi nikamwambia why not, na mimi nikakubali.

Joh makini anasema kuwa baada ya mazungumzo hayo siku iliyofuata ice prince alimtumia baet ya wmbo huu na yeye kufanya yake na kisha baada ya hapo ni kufanya mazungumzo na menejiment yake.

Mwisho wa siku nafanya muziki wangu na ninaamini wapo wanaotupenda na wapo watakao amua kutupenda tu, na wapo watakao amua kutotupenda lakini wapo ambao walitujua since day one kabla hatujawa kina Joh makini.

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.