Baada Ya Kimya Kirefu, Wolper Afunguka Chanzo Cha Kuachana Na Harmonize

Ikiwa ni zaidi ya miezi mitatu kupita tangu penzi la msanii wa bongo movie na mjasiriamli jackline wolper na msanii wa bongo fleva harmonize kuvunjika, wolper aamua kufunguka kuhusu chanzo cha wao kuachana,wolper anasema kwa muda mrefu alikuwa kimya huku watu mitandaoni kila mmoja akisema lake kuhusu wawili hao.Ikumbukwe kuwa ni muda mfupi tu tangu kuachana kwao ,wawili hao kila mmoja alianza kujirusha na mpenzi mpya bila kujali mahusiano yao yaliyopita huku wolper akikiri kabisa kuwa mahusiano yake na harmonize ndio mahusiano yaliyovunjika na kumuuma sana kuliko yote, ikiwa ni mahusiano yake ya nne.

Akiongea katika mahojiano na mwanahabari millard ayo ,wolper anasema sakata lilianza siku ya kumbukumbu yake ya kuzaliwa ambapo yeye alikuwa  Burundi kikazi  na mpenzi wake huyo wa zamani alipost picha yake katika ukurasa wake wa instagram na kumsifia sana lakini cha kushangaza baada ya siku mbili picha ile ilifutwa na alipouliza aliambiwa wanatafuta kiki ya wimbo mpya, wimbo ambao unakwenda kwa jina la  “happybirthday” ulioimbwa na harmonize kwa ajili yake”nimefuta baby nataka tutengeneze kiki ,unajua kuna wimbo mpya nimekuimbia” wolper asimulia.

download latest music    

Hata hivyo wolper anasema kuwa kipindi icho chote harmonize alikuwa tayari ameshaanza mahusiano na mwanamke mwingine anaejulikana kwa jina la sarah, mwanamke ambae alikuwa anamkataza harmonize kupost kabisa picha za jacky mitandaoni, mwanamke yule alpoona wolper anazidi kumpost harmonize mtandaoni alijua kuwa bado hawajaachana ivyo sarah aliamua kumtafuta wolper”mwanamke alikuwa hataki kudanganywa ,alichofanya akanitafuta,alichukua namba yangu ya ofisi instagram”  asimulia wolper. Kipindi icho mwanamke yule alikuwa ameshawatafuta na kuwatumia picha baadhi ya watu wangu wa karibu ikiwepo mdogo wangu, na hata alipomfikia wolpre mwenyewe alimwambia aachane na harmonize maana tayari yuko na mwanamke mwingine”unajua wewe ni kama unajichoresha,endelea na maisha yako,harmonize ana mwanamke na wanategemea kuzaa”  jacky aendelea kusimulia

Hata hivyo Jacky anasema kuwa pamoja na kwamba yeye kingereza  kinampiga chenga lakini cha Sarah kilikuwa kina kona sana,akimaanisha mwanamke mpya wa harmonize hakuwa na kingereza kilichoonyooka.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.