Baada ya kuachia nyimbo mpya, Rich Mavoko afunguka kuhusu kitu anachokifanya kwa sasa

Rich Mavoko ambaye anafanya muziki chini ya Wasafi records hivi sasa anajipanga kuachia album mpya hivi karibuni baada ya collabo yake ya Show me na Harmonize.

Ingawa umaarufu wake sio kama wa Rayvanny na Harmonize muimbaji huyu anajikaza kufikia kiwango ambacho wasanii wote wa Wasafi records wako.

download latest music    

Akizungumza kupitia kipindi cha Top 20 cha Clouds FM kuwa, Rich Mavoko alisema kuwa yeye mwenyewe hufika saa 12 jioni studio ilikufanya kazi hadi saa 12 asubuhi kwa sababu hivi sasa anamipango ya kuachia album ambayo itakuwa yake ya kwanza. Alisema,

“Hii itakuwa albam yangu ya kwanza kubwa kufanya, nilishawahi kutengeneza na watu wangu wa mwanzo ila haikufanikiwa kutoka.”

Hata hivyo kuna matumaini kwamba Rich Mavoko ataendelea kuwavutia mashabiki kwa wingi baada ya project hii yake mpya.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua