Baada ya kumchokora kwa muda Shilole hatimaye amjibu Gigy Money

Image: Shilole amjibu Gigy Money

Hapo awali Gigy Money alisema kuwa yeye sio shabiki wa Shilole wala nyimbo sake. Kulingana na mrembo huyu wa video za nyimbo za Bongo, shilole hajui kuzungumza kingereza vizuri na hii pia ndio maana hatamani kuwa shabiki wake!

Gigy Money

Hata hivyo, Shilole ameamua kumjibu mrembo huyu kupitia 5 Selekt ya EATV alipokuwa akifanyiwa mahojiano. Shilole alionekana kuto jali alichosema Gigy money na kwa sababu huyu ni Mudigi wake….hakuona haja ya kujibazana naye. Shilole alisema;

download latest music    

“Ni mdogo wangu kwa hiyo lazima apite kwa dada yake, kwa hiyo watu kama hao wadogo zangu ninawachukulia poa tu, hamna tatizo,”

Shilole aliendelea kwa kukiri kuwa ni kweli hajui kingereza lakini hilo sio jambo la kumsumbua akili;

“Kingereza is not my language, kwa hiyo nikisema bado hainilazimishi kukijua sana lakini najifunza kuongea, na pale panapobidi nitaongea. Hiyo ni kweli hamna shida kama sijaenda (shule) ni sawa, kwani watu wangapi hawajaenda shule, ukiwa umeenda shule na hela uwenayo.”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua