Baada Ya Kunusurika Kifo, Aunty Ezekiel Arudi Kanisani

Staa wa filamu za kibongo mwanamama Aunty Ezekiel Grayson amerudi kanisani baada ya kunusurika kuchungulia kaburi baada ya kuumwa sana.

Siku chache zilizopita picha zilisambaa zikimuonyesha Aunty Ezekiel akiwa amelala Kwenye kitanda cha hospitali huku akiwa hoi taabani.

download latest music    

Baadae taarifa zilisambaa kuwa Aunty Ezekiel anasumbuliwa na ugonjwa wa Malaria ambao ulimfanya mpaka alalazwa.

Lakini tangu janga hilo litokee Aunty Ezekiel anafunguka na kudai kuwa aliumwa kiasi cha  kudhani kuwa angekufa.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Aunty Ezekiel amekiri kuwa tangia amepona ameamua kwenda kanisa la Katoliki la Kisarawe mkoani Pwani, mahali ambapo alikulia.

Mungu alinitendea makuu kwa kuniinua tena kitandani na kuweza hata kuzungumza hivyo sina budi kumshukuru”.

Aunty Ezekiel alikiri kufanya hivyo kwa sababu alipokuwa akiumwa hakujua kama ataweza kuinuka tena na kuzungumza kama zamani kwani alishakata tamaa, lakini Mungu akamponya hivyo hana budi kumrudishia shukurani.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.