Baada Ya Kushinda Tuzo Mbili Wema Sepetu Alamba Shavu Hili Tena

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Wema Sepetu amelamba  shavu jingine siku ya jana baada ya kutangaza kuwa filamu yake ya Heaven sent itauzwa kwa mfano wa DVD ili kuwafikia watazamaji wengi.

Wema alijishindia tuzo mbili wikiend iliyopita kutoka katika tuzo za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) ambazo ni Muigizaji bora wa kike 2018-2019 na People’s choice Award (Chaguo la watu).

download latest music    

Lakini inaonekana huo ulikuwa mwanzo tu wa baraka za Wema kwani jana kwenye mkutano na waandishi wa habari Wema ametangaza kupata dili jingine na Azam Tv likiwa ni Kusambaza movie yake kwenye mtindo wa DVD.

Tangu movie ya wema imetoka mapema mwaka jana amekuwa akiiuza filamu hiyo kwa mtindo wa digitali kumaanisha amekuwa akiuzia filamu hiyo Kupitia App yake ya Wema Sepetu inayopatikana kwa simu za Android.

Wema amehaidi kufanya filamu full time na kuhakikisha analeta mambo mazuri katika tasnia hii ya Bongo movie lakini pia Kumekuwa na tetesi kuwa mwezi wa Sita ana mpango wa kuzindua filamu yake aliyoigiza na Van Vicker.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.