Baada ya kutangaza anamrudia mungu Sabby Angel aonekana kwenye kumbi za starehe akila bata

Image: Sabby Angel

Msanii anayefanya muziki na filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ alifunguka hivi karibuni na kutangaza kuwa anamipango ya kustaafu kwani alikuwa anahisi kuwa imefika wakati ambao anafaa kumrudia mungu.

Sabby Angel aliwashangaza wengi kwa tangazo hilo wengi na mashabiki wake huku wakiwa na hofu kuwa msanii huyu angepotea kabisa kama wengi ambao waliacha kutumbuiza hapo zamani.

download latest music    
Sabby Angel
Sabby Angel

Lakini inaonekana kuwa Sabby Angel bado hajaamua anachotaka kwa kweli. Hivi karibuni alionekana akijivinjari kwenye klabu wiki kadhaa baada ya kusema kuwa anapanga kumrudia mungu.

Hata hivyo alivyohojiwa na global Publishers msanii huyu alisema…

“Mmh! Sina hata la kujitetea, ukweli nimeamua nimrudie Mungu, lakini haya mambo ya starehe najitahidi kuacha kidogokidogo, hadi pale nitakapoweza kuacha kabisa kwenda klabu na upuuzi mwingine.”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua