Baada Ya Kutoka Gerezani,Babu Seya Kufungua Kanisa

Kila mmoja anakuwa na imani yake na njia yake ya kumshukuru Mungu kwa yale yalimkuta na kumuepusha katika maisha yake, swala la shukurani kwa Mungu linakuwa la kiimani zaidi.Hii pia inatokea kwa wasanii maarufu na waliokuwa wanapendwa sana miaka ya nyuma kutokana na kazi zao za muziki walizokuwa wakifanya, hapa tunawazungumza Babu Seya na mtoto wake Nguza Viking ambao wameachiwa huru December 9 mwaka huu.

Wasanii hao ambao walifungwa mwaka 2004 kwa tuhuma za kulawiti watoto ni mtu na mtoto wake na wamekaa gerezani kwa zaidi ya miaka 12 huku wakiwa na hawana tumaini la kutoka gerezani humo lakini  Mh.rais wa Tanzania aliamua kuwakumbuka na kuona kuwa kifungo walichokitumikia kitakuwa tayari kimewafunza kitu.

download latest music    

Wengi wamekuwa wakitoa ushauri kuwa wasanii hao bado wanahitajika sana katika jamii na katika soko la muziki huku mashabiki wakionyesha kiu zao za kuwataka kuwasikia tena katika muziki wakifanya vizuri kama mwanzo,lakini hata baada ya kutoka wasanii hao wamekuwa kimya kwa muda na hawakutaka kuongelea chochote kuhusu swala hilo.

Jana katika ukurasa wa Twitter unaosemekana kuwa ni wa kwao wasanii hao walithubutu kusema kuwa njia rahisi walioichagua ya kuamua kumtukuza Mungu na kumuonyesha shukrani kwa Mungu wo ni kuamua kufungua kanisa ikiwa ni jambo walilokuwa wamepanga siku nyingi tangu wakiwa gerezani endapo wangepata nafasi ya kutoka humo.

Mwaka mmoja kabla ya kuipata hii neema ya msamaha kunipata kuna mfungwa mwenza alipata kuniuliza  ukitoka utaendelea kuimba, nilichomjibu ni kua nikitoka ntafungua kanisa nimtukuze Mungu  naaam hata sasa nitafungua kanisa.

Ingawa wamejitokeza watu wengi hasa mapromota wakitaka kufanya kazi na watu hao lakini bado wao hawajatoa msimamo wao kabisa kuwa baada ya hapo wanataka kufanya nini.Wasanii hao walitamba sana enzi zao na kibao cha baba na mwana.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.