Baada Ya Kutuma Maombi kwa Mh. Rais ,Lungi Amshambulia Ray C

Wiki chache zilizopita msanii wa kike Rehema Chalamila maarufu kama Ray C alimuandikia Mh.Rais Magufuli barua na kumuomba  kuweka sheria ya kuzuia ufuksa katika nyumba za kulala wageni kwa kutunga sheria itakayo waamuru   watu wanaoingia katika nyumba za wageni wawe ni wale waliofunga ndoa  na wanapofika maeneo haya watoe na vyeti vya ndoa kuthibitisha kuwa wana ndoa iliyo halali. Msanii mwenzie Lungi Maulanga amemjibu na kumshambulia kuwa maneno hayo ameyasema kwa sababu hana ndoa na hayajawahi kumkuta yanayowakuta.

Msanii huyo wa kike anasema kuwa Ray C hakupaswa kuyaongea hayo ilhali hana ndoa alipaswa kuyaongea haya siku akiwa ameshaingia katika ndoa na ameyaona yanayopatikana katika ndoa ndio aweze kusema hayo yote.

download latest music    

ninavyomjua ray c ni kwamba hajaolewa sasa hayo anayomwambia mheshimiwa anatakiwa kuyafanyia kazi kwanza yeye kwa sababu ninachoamini kuwa hata yeye bado anaingia katika nyumba za wageni na wala hajaolewa.anatakiwa atupe mfano kwnza kutoka kwake  sababu najua sheria hatungi yeye. Alifunguka Lungi

Hata hivyo majibu ya Lungi kwa Ray C haijafamika kama amemjibu kwa ugomvi au ni kitu gani kilimkera kutoka kwa maoni ya msanii mwenzie huyo ilhali haijawahi kuripotiwa kwamba wawili hao walishawahi kuwa na mgogoro wowote kabla.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.