Baada ya ‘Muziki’ Darassa apanga kuachia nyimbo mpya

Darassa ambaye anatambulika Afrika Mashariki amewahaidi mashabiki wake nyimbo mpya ambayo aitawachilia hivi karibuni. Nyimbo hii inakuja miezi mitano baada ya kuachia Muziki ambayo imefanya vizuri baada ya kuangaliwa mara 7,056,225 YouTube.

Nyimbo hii ambayo inaitwa Hasara Roho ndio itakuwa project yake ya kwanza mwaka huu na mashabiki wake wameonyesha furaha kwani wameigonja project nyingine kutoka kwa Darassa.

download latest music    
Darassa

Kupitia Instagram yake Darassa aliandika kusema,

“Good morning from Bongo Tanzania East Africa to the Top of the world!. Nataka kusema asanteni sana kwa love na support ambayo mmetupatia kwenye project yetu ya ‘Muziki’ na kuipelekea kuwa National Anthem. Hakuna neno linaweza kumaanisha thamani yenu kwetu! God bless you all usikose kusikiliza project yetu mpya leo ??? #CMG#HasarARoho,”

Hanscana ambaye ni mmoja wa manager wake aliambia Bongo5,

“Sisi tumejiandaa vizuri kwa sababu tunajua mashabiki wanataka nini. Maandalizi ni makubwa sana, yaani ni kama tunaandaa Marais 5 wa nchi. Kwahiyo tumejipanga vizuri kuhakikisha jamaa anarudi vizuri katika game,”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua