Baada Ya Tetesi Za Kusainiwa WCB, Barakah The Prince Azungumza

Mwanamuziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amefungukia tetesi ambazo zimekuwa zikisambaa kwa muda mrefu sasa kuwa amejiunga na label ya WCB.

Tetesi za Barakah kusainiwa WCB zilianza kushika kazi siku za hivi karibuni baada ya kuonekana ana ukaribu na wasanii wa label hiyo na hata wadau wa WCB.

download latest music    

Lakini tetesi hizi ziishika hatamu zaidi pale Barakah alipodaiwa kutengeneza kiki ya uongo ya Rommy kumtongoza mpenzi wake Naj ilimradi watangaze ngoma yao mpya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Rick media, Barakah The Prince amekana tetesi za yeye kujiunga WCB na kudai ni marafiki tu wa karibu:

Hapana, WCB ni kama familia yangu, mara nyingi hata mameneja wa WCB ndio wanakuwa wananiongoza na kunielekeza nifanye nini.

“Kwa hiyo tumeamua kuwa kama familia na kuna wasanii wengi wanafanya vizuri, lakini sio kwamba nipo chini ya WCB, no siyo kweli“.

Hapo nyuma Barakah hakuwa na ukaribu na WCB mpaka pale alipojitoa Kwenye label ya Rockstar 4000 ya Ali Kiba.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.