Baba Diamond na Baba Ommy Dimpoz Warushiana Maneno

Baba mzazi wa Staa wa Bongo fleva Ommy Dimpoz,  Mzee Faraji Nyembo amemtolea povu Baba wa staa Diamond Platnumz, Mzee Abdul Juma kutokana na tabia yake ya kumsema mwanaye vibaya.

Gazeti la Risasi Mchanganyiko  linaripoti kuwa Kwenye mahojiano waliyofanya na Baba Ommy Dimpoz alitoa taarifa ya mtoto wake kuendelea vizuri na kusisitiza hata kama mtoto wake hamsaidii kwa lolote maishani lakini hawezi kumsema vibaya kama Baba Diamond anavyofanyaga kwa mwanaye.

Unajua mimi ni mzazi wa tofauti sana, siwezi kumlalamikia au kumsemea mabaya mwanangu kwenye vyombo vya habari kama anavyofanya baba Diamond, ninachofanya huwa namuombea mwanangu awe na maisha mazuri maana nikimuombea mabaya anaweza kupoteza dira ya maisha yake nitakuwa nimefaidika na nini.

Namshauri baba Diamond awe anamuombea mwanaye mafanikio, aungane naye wawe kitu kimoja, afurahie mafanikio yake ipo siku Mungu atamrudisha kwake amsaidie na siyo kumzungumzia maneno ya kumlaani na kumlalamikia kila siku.

Aige mfano wangu maana mimi huwa simlazimishi mtoto anisaidie bali huwa napambana na hali yangu kwa kufanya kazi kwa bidii na ninampenda sana mwanangu Dimpoz na siwezi kumlaani au kumlaumu maana jina nililompa la Omary ni la baba yangu inakuwaje sasa nimlaani ni sawa na kumlaani baba yangu”.

Baada ya povu hilo gazeti hilo lilimsaka Baba Diamond na kumuhoji kuhusu kile alichosema Baba Dimpoz na alimwaga povu hili:

download latest music    

Sitaki shobo, huyo baba Dimpoz simfahamu kama hana la kuongea anyamaze, amzungumzie mwanaye hata kama niliongea kuhusu Diamond si mtoto wangu yeye inamuhusu nini?”.

Kuhusu huyo Diamond sihitaji kuzungumza chochote kuhusu yeye wala watoto wangu maana hawana faida yoyote kwangu kwa sasa”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.