Baba Dimpozi Afananisha Malezi ya Ommy na Tatizo la Wema

Baba mzazi wa Ommy Dimpoz ambae juzi alifunguka na kusema kuwa hataki kusikia wala kumuona mwanae huyo akija katika mazishi yake siku ya kifo chake kwa sababu mtoto huyo amekuwa hamjali hata kidogo kipindi cha uhai wake ilhali mtoto huyo sasa hivi ana hali nzuri kimaisha na anashindwa kumkumbuka baba yake.

Swala la wazazi kulalamika kuhusu watoto wao hasa wasanii limekuwa sio swala geni katika tasnia kwa sababu tatizo hilo limekuwa likiibuka kila kukicha na kama utakumbuka ni hivi juzi juzi tu baba mzazi wa msanii mkubwa Dimaond Platinumz alitamka maneno ya hasira sana kwa mtoto wake huyo wa kiume.

download latest music    

Baba Ommy Dimpoz anasema kuwa pamoja na kwamba anahisi kosa lake ni kutokujihusisha na malezi ya Ommy Dimpozi kipindi cha ukuaji wake lakini anaamini kuwa hata swala la kumleta Duniani tu ilikuwa ni swala tosha la mtoto huyo kumjali na kuheshimu.

Hata hivyo baba Ommy Dimpoz anasema kuwa amekuwa akisikia jinsi Wema Sepetu ambavyo  anahangaika kupata mtoto lakini mwisho wa siku unaweza kukuta mtoto huyo  akashindwa kumsaidia mama yake lakini hiyo haibadilishi swala ya yeye kuwa mzazi.

mfano kama nikifa leo wala asije kunizika au kukanyaga Tabora , kwanza akija atasema nani amefariki, watampiga maana kipindi niko hai tu wala hanijali.Ni kama Wema Sepetu sasa hivi anavyohangaika kutafuta mtoto siku hakimpata hata kama hawezi kumsaidia lakini bado atamshukuru Mungu tu na mimi ni hivyohivyo, huwa namshukuru Mungu kuwa nimemleta Ommy Duniani.-Alifunguka baba huyo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.