Baba Kanumba Afurahishwa na Kitendo Cha Lulu Kutoka Gerezani

Baba mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Steven Kanumba, Charles Kusekwa Kanumba amefunguka na kuweka wazi furaha yake baada ya Lulu kuachiwa gerezani kupewa kifungo cha nje.

Tofauti na Mama Kanumba ambaye aliweka wazi kuwa alikasirishwa na Kitendo Cha Lulu kuachiwa huru, Baba Kanumba ameweka wazi kuwa hana neno na Lulu na amefurahi alivyotoka kwani hata kama angefungwa miaka 100 mwanaye hawezi rudi.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Ijumaa Wikienda Baba Kanumba amesema yeye ni mcha Mungu hivyo hawezi Kubeba kinyongo dhidi ya Lulu.

Kila kitu hapa duniani hupangwa na Mungu na kila kinachotokea ni mapenzi yake, siwezi kulaumu kwa nini Lulu ametoka bali nimefurahi kwa sababu hata angefungwa miaka mia moja, Kanumba tayari alishafariki dunia, hawezi kurudi duniani.

Silaumu kwa sababu mimi ni mcha Mungu hivyo Mungu ndiye amesema suala hilo lifikie tamati kwa namna hiyo, wanaopinga na kusema siyo haki, hayo ni mawazo yao maana kama ni kifo cha mwanangu kiliniuma sana, lakini sasa siwezi kumlazimisha Mungu afanye mimi binadamu ninavyotaka maana hata neno lake linatufundisha kwamba tusamehe“.

Lakini pia Baba Kanumba amempa masharti mazito  kwamba kama anataka maisha yake yaende vizuri, awe na familia nzuri kama watu wengine na amani moyoni, anatakiwa kwenda kufanya usafi kaburi la Kanumba kama ni kulia, alie na hapo atakuwa ameacha balaa na mikosi yote.

Kwa mila za kabila letu la Kisukuma ni kwamba, Lulu alitambulika kama mke wa Kanumba maana hakuna mwanamke mwingine tunayemfahamu sisi hivyo natamani angeachiwa huru kabisa asiwe na kifungo cha nje na aende tu kufagilia kaburi la mumewe Kanumba na hapo atakuwa amemaliza na kuwa huru.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.