Baba Levo Aburuzwa Mahakamani Baada Ya Kumtembezea Kichapo Muuguzi

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Crayson Revocatus Chipando maarufu kwa Jina la usanii kama Baba Levo amejikuta katika upande mbaya wa sheria baada ya kumtembezea kipigo muuguzi.

Baba Levo mbali ya kuwa msanii Lakini pia ni mwanasiasa ambapo sasa ni diwani kata ya Mwanga Kaskazini, Kigoma Ujiji.

download latest music    

Siku ya jan Baba Levo alifikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kigoma kusikiliza hukumu ya kesi inayomkabili ya kumpa kipigo muuguzi wa Zahanati.

Azam Tv wanaripoti kuwa Msanii huyo ambaye pia ni Diwani kwa tiketi ya ACT Wazalendo anatuhumiwa kufanya makosa matatu ikiwemo kutumia lugha ya matusi, kumshambulia na kumfanyia vurugu muuguzi wa zahanati ya Msufini iliyopo kata ya Mwanga Kaskazini.

Kesi hiyo imehairishwa mpaka tarehe 19 September ambapo itasikilizwa tena.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.