Babu Seya, Papii Kocha na Familia Watinga Ikulu Kumuangukia Raisi Magufuli

Mwanamuziki wa muziki wa dansi, Nguza Viking au maarufu kama Babu Seya pamoja na watoto wake Johndon Nguza ‘Pappii Kocha’, Francis Nguza na Michael Nguza ambao waliwasili Ikulu leo tarehe 02 January kwa ajili ya kumshukuru kwa msamaha alioutoa kwao dhidi ya kifungo cha maisha walichokuwa wanatumikia.

Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanae Papii Kocha walihukumiwa kifungo cha maisha miaka kumi na nne + iliyopita lakini baada ya kutumikia kifungo chao cha maisha kwa miaka kumi na nne mapema mwaka huu kwenye sherehe za Uhuru Raisi Magufuli aliwatangazia msamaha kutoka katika kifungo chao cha maisha na kuachiwa huru.

download latest music    

Siku ya leo familia nzima ya Nguza Viking wameongozana na kutinga Ikulu ambapo wameweka wazi kuwa wameenda pale kwa ajili ya kumshukuru Raisi kwa msamaha aliowapa na kuwaacha huru na pia wameenda Ikulu kwa ajili ya kuomba ruhusa na kupata baraka ya kuendelea na kazi.

Baada ya kumaliza makutano yao na Raisi Magufuli Babu Seya alifunguka yafuatayo kuhusu makutano yao na Raisi:

Yaani sijui niseme nini hapa nilipo nina furaha sana moyoni mwangu, nilikuwa naomba tangu muda mrefu nikutane na Raisi Magufuli, nimeomba sana mpaka leo nimefanikiwa kukutana naye na nimemwambia namshukuru sana kwa kutusamehe na hivi sasa nipo tayari kuchapa kazi, hapa kazi tu”.

 

 

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.