Babu Tale Afunguka Baada Ya Tetesi Za Kumtelekeza Hawa India

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka baada ya maneno maneno kusemwa kuwa amemtelekza mrembo Hawa Said nchini India ambako anapata matibabu.

Wiki mbili zilizopita Babu Tale alimpeleka msanii Hawa kwa ajli ya matibabu nchini India baada ya kuifanyiwa vipimo na upasuaji mkubwa Babu Tale amerejea nchini siku chache zilizopita na kumuacha mgonjwa Nchini India.

download latest music    
.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Babu Tale alisema amerejea nchini na kumuacha Hawa India kwa kuwa msanii huyo anaendelea vizuri hivyo baada ya kushauriana na madaktari wake walimwambia asiwe na wasiwasi mgonjwa yupo sehemu salama hakuna ulazima wa yeye kuendelea kumsimamia muda wote.

Madaktari ndiyo walioniruhusu nirudi Bongo na wakanihakikishia hali ya mgonjwa wangu inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo hivyo hakuna ulazima wa mimi kuendelea kuwepo muda wote kama nitahitajika kwa lolote watanijusha.

Baada ya kupata kauli ya wataalamu hao nikaona nirudi nije kuendelea na mambo mengine huku nikiwasiliana nao kiukaribu zaidi”.

Hawa alipelekwa nchini India ambako walienda wakidhani ana ugonjwa wa ini lakini walikuta ana gonjwa wa moyo hii ni baada aliyekuwa mpenzi wake miaka ya nyuma msanii Diamond Platnumz kujitolea msaada huo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.