Babu Tale Bado Anatusimamia Tip Top Pamoja na Kuwa Bize WCB- Dogo Janja

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja amefunguka na kukiri kuwa Babu Tale bado anawasimamia wasanii wa Tip Top pamoja na kuonekana sana WCB.

Babu Tale ambaye kwa sasa ni Meneja wa staaa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, lakini ni mmoja kati ya waanziloshi wa label ya kitambo ya Tip Top yenye wasanii nguli kama Madee, Dogo Janja, Kassim Mganga na wengineo.

download latest music    

Lakini tangu Babu Tale apate mafanikio katika label ya WCB Kumekuwa na tetesi kuwa amewatelekeza wasanii wote wa Tip Top baada ya kuonekana sana WCB tetesi ambazo Dogo Janja amezikana.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa hilo halina ukweli wowote kwani wamekuwa wakishirikiana kwa mambo mengi.

Hapana sio kweli, Babu Tale anasimamia kazi zangu sana sana ila kwamba huku Tip Top sisi hatuko bize kama Wasafi ndio maana unaoa muda wote yupo kule, hatuna matukio.

Lakini nikiachia wimbo utaona redioni nitaenda na Babu Tale, so mimi sina matukio mengi ndio maana kwenye kazi zangu anakuwa mara chache sana pale ninapomuhitaji”.

Dogo Janja hivi sasa chini ya Label ya MMB (Manzese Music Baby) ambayo iko chini ya msanii mkongwe Madee Ali.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.