Babu Tale Kamchana Ruby Kuwa Siku Akigundua Tatizo Lake Akajirekebisha Basi Heshima Yake Itarudi

Mdau mkongwe katika sanaa ya Bongo fleva Babu Tale na maarufu zaidi kwa kuwa meneja wa mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz, amefunguka na kumchana msanii Ruby kuhusu tatizo alilonalo.

Ruby ambaye ni mwanamuziki wa Bongo fleva alifanya vizuri zaidi na vibao vyake mbali mbali siku za nyuma kidogo kwa kipindi cha mwaka mzima Ruby amekuwa kimya bila ya kutoa ngoma yoyote zaidi ya kuonekana kwenye mitandao ya kijamii jambo alilolieleza kuwa amechukua mapumziko kidogo.

download latest music    

Mziki wa Ruby ulianza kulega lega pale alipoamua kujitoa kwenye jumba la vipaji Tanzania (THT) ambapo sanaa yake mwanzoni kabisa aliianzia kwenye jumba hilo lakini mwishoni alipishana kidogo na mabosi zake huko THT  na kuamua kujiengua.

Siku ya Jana kuna video clip iliyomuonyesha Ruby akiimba wimbo wa dini wakusifu kwa hisia kali ambapo wasanii mbali mbali walikiri kuikubali sauti yake na kukikubali kipaji chake wakiwemo Kajala, Jacqueline Wolper, Shetta, na pia Babu Tale.

Babu Tale kupitia ukurasa wake wa Instagram aliiposti video hiyo na kuisindikiza na ujumbe uliomtaka Ruby kujua anasumbuliwa na ugonjwa gani kulitatua na kisha atapata heshima yake kwenye muziki anaofanya:

Fundi Sana we binti siku ukijua unaumwa nini na ukaamua upone basi ujue heshima ya wote wanao kuchukulia poa itarudi kwako Helena mama mimi nakuzimia unajua hilo mimi ni mmoja wa watetezi wako popote ulipo mama”.

Hii ndio video clip ya Ruby iliyozua gumzo siku ya Jana mtandaoni:

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.