Babu Tale na Hawa Wazuiliwa Kwenda India Kwa Matibabu

Aliyekuwa Msanii wa Bongo fleva Hawa Said alimejikuta akizuiliwa kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu baada ya kutokidhi vigezo vya kusafiri na Kurudisha katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA).

Diamond alitangaza kutoa pesa kwa ajili ya matibabu ya Hawa ambayo ni jumla ya shilingi Milioni 450 katika kuvhukua jukumu la kumsaidia katika kipindi kigumu alichokuwa nacho.

download latest music    

Katika mahojiano aliyofanya na Maananchi Communication Limited baada ya kukwama  Oktoba 13, 2018 meneja wa Diamond Platnumz Babu Tale amesema hali hiyo imewakuta wakiwa tayari wameingia ndani ya uwanja wa ndege na kuanza kukaguliwa nyaraka zao mbalimbali.

Babu Tale amesema nyaraka iliyowakwamisha kusafiri ni kibali cha daktari kuelezea hali ya mgonjwa ili wahudumu ndani ya ndege wajue namna watakavyomhudumia.

Kuna mgonjwa anaweza akawa katika hali ya kuzimia, kutapika anatakiwa ahudumiwe tofauti, hivyo Hawa imeshindikana kwa kuwa hakuna hizo nyaraka inayoonyesha hivyo kutoka kwa daktari na wametwambia turudi itakapokamilika,

Hawa, Babu Tale na mama yake, Ndagina Hassan ilikuwa waondoke leo saa 10:45 na ndege ya Shirika la Emirates lakini walikataliwa kusafiri baada ya kutotimiza vibali vya kusafiri vya kimatibabu kwenda India.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.