Baby Madaha Adaiwa Kutimuliwa Kwenye Nyumba Ya Kupanga Baada Kushindwa Kulipa Kodi

Mwanamuziki wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na wimbo wake wa ‘Amore’ Baby Madaha amefungukia tetesi za yeye kutimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa amepanga baada ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba hiyo.

Habari zimetapakaa mtandaoni kuwa Baby Madaha amefulia vibaya kiasi ya kwamba hajiwezi hata kulipa kodi ya nyumbani kwake alipopanga jambo lililomlazimu kuhamia kwa shoga yake Isabela Mpanda ‘Bela Fastaa’ maeneo ya Mbezi Beach.

download latest music    

Taarifa za chini ya kapeti za kimbea zaidi zimedai kuwa mambo yamemuendea kambo staa huyo hii ni kutokana na ukimya wake Kwenye muziki hasa kushindwa kutoa hit song na biashara zake zimebuma jambo linalompelekea kufulia kufika hadi hatua ya kukosa pesa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari Baby Madaha amekataa kata kata tuhuma hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote:

Hayo ni maneno tu ya watu waliokuwa na chuki na mimi si kweli kama nimefulia na ifahamike kuwa siku nyingi nakuwa niko Dubai nafanya shughuli zangu ninapokuja Tanzania na kufikia kwa Bella siyo tatizo”.

Lakini pia Baby Madaha amedai kuwa yeye haishi Dar kwa sasa kwaiyo haitaji nyumba hivyo akifikia kwa marafiki sio mbaya:

Nilirudi Bongo hivi karibuni kwa ajili ya harusi ya mdogo wangu na siishi hapa kwaiyo suala la kushindwa kulipa kodi na kuenda kuishi kwa Bela halina mshtuko”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.