Baby Madaha aeleza sababu yake ya kurudi nyumbani kuwaona wazee wake kila mwaka

Image: Baby Madaha

Muigizaji wa muvi za Bongo, baby Madaha Joseph hivi karibuni alikiri kuwa kila mwaka yeye hurudi nyumbani kwao kila mwaka kuwaona wazazi na wazee wake wanaoishi mashinani.

Baby Madaha

Mrembo huyu alifunguka kudai kuwa true hufanya jambo hili ilimambo yake yaendelee kwanda vizuri. Kutembea kwa wazazi ‘kutambika’ ni jambo muhimu kulingana na Baby Madaha ndio apate baraka.

download latest music    

Aliambia kipindi cha Motomoto new kuwa hivi sasa yuko nyumbani kwa wazazi wake baada ya kukaa sana mjini bila kuwaona.

“Bila wazee mambo hayaendi kabisa, niko kwetu Mwanza kwa ajili ya kufanya mambo ya kimila ili walau mambo yaende vizuri mjini maana hali imekuwa mbaya sana, nimekuwa nikifanya hivyo kila mwaka na nimeona huwa inasaidia sana,”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua