Baby Shower ya Mtoto wa Gigy Money Majanga

Video queen aliyegeukia muziki wa Bongo fleva na kusumbua vibaya mno na kibao chake cha ‘Nampa papa’ Gigy Money amepata wakati mgumu baada ya aliyotarajia kumfanyia mtoto wake aliye tumboni kuota mbawa.

Gigy Money aliushangaza ulimwengu alipotokea ofisi za Basata alipoitwa na Waziri Julianna Shonza akiwa na ujauzito mkubwa wa miezi saba aliouficha kwa muda mrefu.

download latest music    

Lakini tangu ujauzito wake auweke wazi pia Gigy Money amepitia majanga mengi sana ikiwemo kuweka wazi kwenye mtandao wa kijamii kuwa baba mtoto wake ambaye ni mtangazaji wa Choice Fm, Mo Jay anatabia ya kumtembezea kichapo.

Gigy Money alikiri kuwa mpenzi wake huyo anampiga wakati yu mjamzito kitendo alichodai kimempelekea kufikia uamuazi wa kuachana naye na kuwa single mama, uamuzi ambao ulidumu kwa siku chache kwani baadae walirudiana.

Baada ya kuwa katika nafasi nzuri na baby daddy wake Gigy alianza kuandaa baby shower yake kabla hajajifungua mwezi ujao lakini amejikuta anashindwa kufanya shughuli hiyo kutokana na mambo ya kifedha kutokaa vizuri.

Habari za chini chini zimekuwa zikidai kuwa Gigy alikuwa hana mpango wa kufanya baby shower kwa muda huu alikuwa anasubiri mpaka atakapo jifungua lakini baadhi ya marafiki zake wakamshawishi aifanye jumamosi iliyopita lakini siku zilipokaribia hali ya kiuchumi ilikuwa mbaya kidogo.

Baada tetesi hizi kusambaa gazeti la Global Publishers lilimtafuta kwa ajili mahojiano na alifunguka haya:

Nilikurupuka kuandaa shughuli ndani ya wiki moja wakati nataka iendane na hadhi ya jina langu, nikaona isiwe tabu nikasogeza mbele hadi wiki ijayo”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.