Bahati Ampongeza Diamond kuwa Msanii wa Kwanza Kuanzisha Lebo

Msanii wa muziki wa injili kutoka nchini kenya,Bahati amemsifia na kumpongeza msanii mkubwa bongo na afrika kwa ujumla Diamond Platinumz kuwa msanii wa kwanza Afrika kuanzisha lebo na kuwainua wasanii wengi we waliokuwa na vipaji na wakakosa watu wa kuwapa sapoti.

Bahati ambae nae pia amekuwa na lebo yake ya kutengeneza wasanii wanaochipukia inayojulikana kama EMB, amesema kuwa Diamond ni mfano wa kuigwa kwa sababu ameweza kuanzisha na kuisimamaia lebo hiyo na kuweza kufanikiwa kujulikana kila sehemu na watu wengi sasa wamekuwa wakifata mfano kutoka kwake.

download latest music    

Akijitahidi kumfananisha Diamond na wasanii wengine wa nje , Bahati anasema kuwa wasani wakubwa kama kina Chris Brown hawajaaanzisha lebo kwa miaka yote waliokuwepo katika muziki kwa sababu kuanzisha lebo na kuipa muda wa kukua na kuimarika ni kazi sana sio kama watu wanavyodhani .

Nataka kutoa shukrani nyingi sana na kumpongeza sana founder wa wasafi,Diamond Platinumz.unajua watu wanatoka lebo nyingi lakini wansahau kum-thank huyu mtu  na kum-acknowledge the visionary wa Afrika  Diamond kwa kuwa msanii wa kwanza kuonyesha na kuanzisha lebo na kusema zinaweza work .so big up kwanza kwa Diamond na vision yako ya Wasafi 

Bahati pia anawaomba wasanii wengine wanaotaka kuanzisha lebo wafanye kwa kuwa na vision ya kuanzisha lebo na sio kufanya tu kwa kuwa diamond au nani amefanya basi na mimi nifanye.

Napenda kuwapa neno pia wasanii wengine wanaotaka kuanzisha lebo kuwa wanapotaka kuanzisha lebo waw na vision na sio kwa sababu diamond amefanya au bahati kafanya,utajikuta unapoteza ela nyingi sana lakini hautaweza kupata vingine , lakini kikubwa utapata ambacho ssio cha muhimu sana ni likes za instagram tu.lakipi unapoanzisha lebo ni lazima uwe na roho ya kusaidia na kushikana mkono ili kuinua wengine.-Aliongea Bahati

Bahati alishawahi kufanya nyimbo  na moja ya wasanii wanaotoka katika lebo hiyo ambae ni Rayvanny na wimbo wao uliweza kufanya vizuri.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.